Hadidu za rejea za kongamano la kwanza la vuguvugu la wanaharakati wa Afrika

Kumbukumbu za kihistoria

Taifa la kwanza la Kiafrika katika historia ni Himaya ya kale ya Farao iliyotokana na muungano wa Misri ya nyanda za Juu na Misri ya nyanda za Chini, kando kando ya bonde la mto Nile. Ni katika zama za kisasa ambapo mataifa makubwa ya kiafrika (Ghana, Zimbabwe, Mali, Songhay nk) yalipoteza uhuru wao kutokana na mashambulizi ya pamoja ya wa Almoravid na Wareno. Baada ya kudhoofika kwa kiasi kikubwa kutokana na biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki, jangwa la Sahara na bahari ya Hindi, waafrika hawakuwa na uwezo wa kupambana na uvamizi na utawala wa kikoloni wa wazungu katika karne ya 19. Ni katika hali hiyo ambapo “mwafaka wa kibeberu” uliotokana na Mkutano wa Berlin wa mwaka 1885 uliochochea kugawanywa kwa bara letu la Afrika, na hali hiyo bado inaendelea hadi leo.
Hata hivyo, kwa kuwa ukagandamizaji wa aina yoyote unachochea upinzani, ujasiri na mapambano ya waafrika dhidi ya aina mbalimbali za utawala wa kigeni (biashara ya utumwa, utumwa wenyewe, ukoloni, ubaguzi wa rangi nk) vilipelekea mwanzoni mwa karne ya 20 kuwa na vuguvugu lilizopangiliwa vizuri na madhubuti: yaani vuguvugu la wanaharakati wa Afrika.
Toka kipindi cha kuanzishwa kwa kongamano la kwanza (1900) huko London hadi kongamano la sita (1974) ililofanyika mjini Dar es Salaam, na hususani kipindi cha kati ya vita kuu mbili za dunia, na hususani wakati wa kongamano la tano huko Manchester (1945), Wanaharakati wa Afrika walifikia malengo makuu mawili ya kihistoria:
 Kuonyesha mwelekeo wa kisiasa, kuweka malengo na mikakati ya kupambana na ubeberu, ubaguzi, na kuwafanya waafrika walio ndani na nje ya bara la Afrika kutambua hatima yao
 Kuanzisha uhusiano kati ya viongozi wa Afrika, Amerika na Karibiani kwa ajili ya mapambano yaliyokuwa yanaendelea duniani kote.
 
Hakika sio kwa bahati mbaya kuona Mwasisi wa Taifa huru la Ghana, Kwame Nkrumah (1957), kuwa mmoja wa makatibu wa Kongamano la Manchester !
Hata hivyo, ni baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, pamoja na ukandamizaji uliokithiri, mapambano ya kudai uhuru na vuguvugu la wanaharakati wa haki za kiraia
waliwalazimisha wakoloni kuanzisha mchakato rasmi wa kufikia kikomo cha ukoloni. Hatimaye harakati hizi zilipelekea, hususani baada ya ushindi wa "Hapana" wa kura ya maoni dhidi ya ukoloni wa kifaransa chini ya uongozi wa raisi De gaulle, huko Guinea mwaka 1958, kulitokea wimbi kubwa la kujitangazia uhuru kuanzia mwaka 1960. Kuanguka kwa ngome za mwisho za ubaguzi wa rangi katika miaka ya 1990 huko Namibia na Afrika Kusini, kulihitimisha kipindi cha kihistoria, ambapo mwanzoni mwa karne ya 20, wazungu walitawala karibu bara lote la Afrika, isipokuwa Ethiopia na Liberia
Hali ya kutokamilika kwa ushindi wa harakati za kudai uhuru wa nchi za Afrika zilizoongozwa na Kongamano la Kitaifa la Kiafrika (ANC) katika makoloni ya kiingereza na Umoja wa Kidemokrasia wa Kiafrika (RDA) katika makoloni ya kifaransa (pamoja na mapambano ya silaha katika makoloni ya kireno, Algeria, Cameroun na Zimbabwe). kwa hakika, kilichotokea baada ya kumalizika kwa kipindi cha ukoloni barani Afrika kilitawaliwa na mapambano yasiyoisha kati ya viongozi wazalendo waliokuwa wanataka kupatikane uhuru kamili wa watu wao kwa upande mmoja, na wale waliokuwa wanapendelea kuendeleza utegemezi wa kiuchumi, kijeshi na kidiplomasia kwa watawala wao wa zamani au wa sasa wa kikoloni. Sio kashfa kusema kwamba kukaa kwao madarakani kwa muda mrefu kulitokana na utiifu wao kwa mabwana wakubwa zao kutoka “Dunia huru/ nchi za magharibi” wakati wa kipindi cha “vita baridi”.
Mwaka 1963, wakati wa Mkutano wa kilele wa kuanzisha Umoja wa Nchi Huru za Kiafraika (OAU) kulitokea mvutano katika makundi mawili pinzani yaliyojulikana kama Casablanca na Monrovia, ambapo la kwanza lilikuwa lenye "msimamo mkali” na la pili lilikuwa na "msimamo wa wastani” kuhusiana na kuundwa kwa Shirikisho la Umoja wa Bara la Afrika. Kutokana na mwafaka wenye mashaka, ulipelekea harakati za umoja wa Afrika ziwe mikononi mwa “makundi ya viongozi wanafiki” na kuweka kalenda ya mikutano ambayo haikuwa na tija, hii ilipekea kushindwa kwa mara ya pili kwa wanaharakati wa umoja wa Afrika, mara ya kwanza harakati za kuheshimu mipaka kama ilivyoachwa na mkoloni zilishindikana kabla ya kupata uhuru. Umoja wa Afrika ulishindwa kuheshimu moja ya kanuni za kuanzishwa kwake yaani “kufuta mipaka iliyorithiwa kutoka kwa wakoloni” kama ilivyojionyesha, kwa mfano, kwa kujitenga kwa Eritrea na kugawanywa kwa Sudan, mafanikio yake ni kutokana na Kamati yake ya Ukombozi iliyosaidia mapambano ya silaha, hususani dhidi ya wareno, ambayo
yalipelekea kuanguka kwa utawala wa kifashisti huko Lisbon na utawala wa wabaguzi wachache huko Kusini mwa Afrika.
Ukiondoa baadhi ya visiwa (Canary, Ceuta, Melilla, Mayotte nk..), mchakato rasmi wa harakati za kupigania uhuru wa Afrika ziliendeshwa vizuri na OAU
Hata hivyo, katika nyanja ya kiuchumi, pamoja na kupitishwa na Mkutano wa Wakuu wa nchi mwaka 1980 kwa Mpango Kazi wa Lagos, ambao ulikuwa ni matunda ya kujifunza kutokana na miongo miwili ya maendeleo duni, Mpango huo ulipata upinzani kutokana na utekelezaji wa “sera za mabadiliko ya kiuchumi” kwa maelekezo ya taasisi za Bretton Woods (Shirika la Fedha Duniani - IMF - na Benki ya Dunia - WB -) "Muafaka wa kikoloni wa Washington" ulichukua nafasi ya muafaka wa Berlin ambao pamoja na kuwa na majina tofauti, bado uliendelea kutekelezwa licha ya kushindwa kutumika ipasavyo.
Hatimaye, mwisho wa karne ya 20 na kuanza kwa milenia mpya, inabidi kukiri kwamba kubadilishwa kwa OAU na kuwa AU, kwa kufuata muundo wa Ulaya, kumepunguza matarajio ya watu ya mabadiliko ya taasisi ya zamani ambayo ilikuwa kama “Muungano wa Wakuu wa Nchi” na kuwa taasisi jumuishi ya umoja wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi barani Afrika. Katika hali hiyo ni ushindi kwa wapinzani wa harakati za umoja wa Afrika.
Hali ya sasa katika karne ya 21
Katika kipindi hiki, kuna baadhi ya mambo ya msingi yanajitokeza:
ü Kwanza, baada ya nusu karne ya uhuru wa bendera, kushindwa kwa Mkutano wa AU huko Accra (2007) kwenye suala la Umoja wa Mataifa ya Afrika, kunaonyesha kunadhihirisha uharaka wa kubadilisha mtazamo, hata ikibidi mkakati:
ü Halafu, baada ya kuongezeka kwa migogoro ya kivita barani Afrika, ambayo mara nyingi hutumiwa kama kisingizio cha kuingiliwa na mataifa ya kigeni, kwa ridhaa au bila ridhaa ya Umoja wa Mataifa, masuala ya amani na usalama wa ndani na nje wa bara zima la Afrika na watu wake wa ndani hata wale walioko ugaibuni yanahitaji kipaumbele cha hali ya juu
 
Kuongezeka kwa umaskini na kukosekana kwa usawa kunasababisha dhiki, vurugu, ujinga, maradhi pamoja na vifo vya mapema, hususani kwa akina mama na vijana ambao ni sehemu kubwa ya jamii. Haya ni baadhi ya mambo yanayohitaji mabadiliko ya
haraka na ya msingi katika mfumo wa uchumi wa dunia ambao uko kwenye mgogoro wa kudumu
ü Hatimaye, ile dhana ya zamani kwamba “anayeishikilia Afrika anaishikilia dunia” imechochea kuongezeka kwa uporaji uliokithiri wa aina zote za rasilimali watu, maliasili na utamaduni wa bara la Afrika, kwa kuanzia na uporaji wa ardhi na udhibiti wa utajiri wa madini yasiyo na mbadala, achilia mbali unyonyaji wa kifedha unaohusiana na ulipaji wa madeni ya serikali, ubadhirifu au ukwepaji kodi.
 
Kwa kifupi, kutokana na mambo haya, waafrika walio ndani na nje ya bara la Afrika wanapinga na kupambana dhidi ya machafuko na ukosefu wa haki.
Mfululizo wa harakati za wananchi dhidi ya utawala mbaya wa viongozi wachache, unaonyesha kushindwa kwa mfumo uliopo, unaofanya kazi kwa faida ya wageni, wakati una madhara makubwa kwa waafrika walio wengi na watu wengine wenye asili ya moja kwa moja ya Afrika
Cheikh Anta Diop alikuwa sahihi aliposema kwamba “hata ubinafsi wa wazi unapaswa kutupeleka kwenye shirikisho” anaongeza kusema kwamba “ni kutokana na kukubaliana na hali halisi tumeweza kuifikisha Afrika katika hali yake ya sasa, je, hatuoni kuwa sasa ni wakati mwafaka wa kuwa na dhana au ndoto ya kufikirika?” Hii ilikuwa ni mwanzoni mwa miaka ya 1980...
Bila harakati za Afrika kuwa na umoja na mshikamano, hakuna ukombozi kwa waafrika na vizazi vyao
Dira
Dira yetu ni kuwa na Afrika mpya yenye umoja, amani, huru, yenye demokrasia na ustawi, inayochukua nafasi yake kwenye jamii ya watu na shirikisho la mataifa
Dhima
Kuweka mazingira ya kuanzisha upya mwamko na kuendeleza mafanikio ya vuguvugu kubwa la umoja wa Afrika, wenye uwezo wa kuwajumuisha/kuwahamasisha waafrika wote na wale wote wenye asili ya moja kwa moja ya Afrika kupitia taasisi tofauti (vyama vya siasa, vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali nk) na watu binafsi ambao wanakubaliana na mpango wa harakati za umoja wa Afrika na ambao wako tayari kuchangia kuanzishwa kwa Shirikisho la kizalendo na kidemokrasia la Mataifa ya Afrika (USA)

etats africains unis